Rais wa Mali aliyeondolea madarakani Ibrahim Boubacar Keita amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatatu, Januari 17, 2022 akiwa na umri wa miaka 76, familia yake na rafiki zake wamethibitisha kifo hicho na kusema Keita amefariki majira ya saa 600 usiku kwa saa za Afrika Mashariki nyumbani kwake mjini Bamako.
Itakumbukwa kuwa, Miaka miwili iliopita, Keita aliugua kiharusi lakini chanzo cha kifo chake hakijawekwa wazi mpaka sasa.
Keita aliiongoza Mali kwa miaka saba kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2020, wakati alipopinduliwa kufuatia maandamano makubwa dhidi ya serikali kutokana na jinsi alivyolishughulikia suala la Wanajihad.
Mgogoro wa kiuchumi na uchaguzi ulio huru pia ulisababisha maandamano hayo dhidi ya utawala wake. Keita alihusika katika siasa kwa zaidi ya miongo mitatu, akihudumu kama waziri mkuu wa nchi hiyo tangu mwaka 1994 hadi mwaka 2000.
Social Plugin