Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri na Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu.
Akitangaza mabadiliko hayo leo Jumamosi Januari 8, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amesema Nape Nnauye ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Mawaziri wapya watano walioteuliwa ni Nape Nnauye (Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari), Hamad Masauni (Mambo ya Ndani), Dk Pindi Chana (Sera Bunge na Uratibu), Anjelina Mabula (Ardhi) na Husein Bashe (Kilimo).
Rais Samia pia ameteua manaibu waziri wapya katika wizara tano.
Manaibu waziri hao wapya walioteuliwa ni pamoja na Anthony Mavunde (Kilimo), Jumanne Sagini (Mambo ya Ndani) Dkt. Lemomo Kiruswa (Madini), Ridhiwani Kikwete (Ardhi) na Atupele Mwakibete (Ujenzi na Uchukuzi).
Social Plugin