Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA VIFO VYA WATU 14 MTWARA


Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti kufuatia vifo vya watu 14 waliofariki dunia na kujeruhi 22 katika ajali ya barabarani mkoani Mtwara iliyotokea Jumapili Januari 2, 2021 usiku katika Kijiji cha Lidumbe, Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara.

Rais Samia amemtaka Mkuu Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Gaguti kufikisha salamu zake za pole kwa wafiwa wote, ndugu, jamaa, marafiki na anaungana na familia hizo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na amewaombea kwa Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu wore mahali pema peponi, Amina.

Rais Sarnia amevitaka vyombo vyote vinavyosimamia usalama wa barabarani kuongeza juhudi za kudhibiti ajali hasa katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka, na pia amewaasa madereva kufuata na kuzingatia Sheria za usalama barabarani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com