********************
NA EMMANUEL MBATILO, KILIMANJARO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu ameitaka Wizara ya Utamadunu,Sanaa na Michezo kuendelea taratibu,kuvikuza na kuviendeleza VIKUNDI vya burudani za kitamaduni ili vizalishe kazi za mikono za utamaduni.
Ameyasema hayo leo Rais Samia wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni Kilimanjaro lililoandaliwa na uongozi wa machifu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Rais Samia amesema tayari Serikali imeanzisha kanzi data sahihi inayohusu machifu, na imeshaanza kuweka taarifa Sahihi za machifu na mchango wao katika kupamabana na ukoloni.
"Serikali inaendelea kuyabaini maeneo ya kichifu na kimila na kuyatunza ili yawe sehemu za vivutio vya nchi yetu na kuibua, kuimarisha na kuhifadhi majengo na zana za zamani ili zibaki kuwa vielelezo vya Utamaduni wetu ". Amesema Rais Samia.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Paulina Gekul amesema kuna umuhimu mkubwa kwa Watanzania kuendelea kutunza tamaduni zetu na kuachana na tamaduni potofu zinazofanywa na baadhi ya watu.
Amesema Serikali kupitia Wizara yake watandelea kutoa ushirikiano kwa machifu kutunza na kuenzi tamaduni zetu.
Social Plugin