SHEIKH WA MKOA WA DODOMA ALAANI MAUAJI ...'HAIKUBALIKI KATIKA JAMII'

 

Sheikhe wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu 

Na Dotto Kwilasa-Malunde 1 blog, DODOMA

Sheikhe wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu amelaani vikali mauaji ya watu watano yaliyotokea katika kijiji cha Zanka Wilayani Bahi Mkoani Dodoma ambapo amewataka watanzania kuwa na roho za huruma pamoja na kukemea vitendo hivyo.

Akizungumza  leo Januari 28,2022 wakati akitoa hotuba katika swala ya Ijumaa katika msikiti wa Gadafi Jijini Dodoma Sheikhe Rajabu amesema jambo hilo halikubaliki na jamii inatakiwa kukemea vikali ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi kwa wahusika ili waliofanya jambo hilo waweze kukamatwa.

“Waislamu tunatakiwa tuwe na huruma,binadamu anatakiwa awe na huruma,tupendane,hili lililotokea  Zanka halikubaliki lazima tukemee kwa nguvu zote na wahusika,uislamu ni dini ya huruma ni dini ya kusaidiana tusaidiane katika hili,”amesema.

Hivi karibuni katika kijiji cha Zanka yalitokea mauaji ya watu watano wa familia moja  wakiwemo Baba,Mama,watoto wawili na mjukuu huku Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma likidai upepelezi bado unaendelea kuwabaini waliofanya tukio hilo.

Kutokana na hali hiyo,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. Philip Mpango ametoa siku saba kwa Jeshi la Polisi kuwatafuta na kuwakamata wale wote waliohusika na tukio hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post