Klabu ya Simba imezindua jezi zao mpya leo Jumatatu, Januari 3, 2022, kuelekea mchezo wao katika Michuano ya Mapinduzi Cup.
Jezi hizo zimezinduliwa visiwani Zanzibar na Afisa Habari wa Klabu hiyo Ahmed Ally, na zitatumika katika michuano ya Mapinduzi Cup na Kombe la Azam Sports (ASFC).
Kwa sasa Jezi hizo zinapatikana madukani yote ya Vunja Bei, Afisa habari huyo amewaomba wanasimba kujipatia jezi mapema.
Akizungumzia uzinduzi huo, Afisa Habari Simba SC, Ahmed Ally amesema; “Tumezindua jezi mpya ambazo tutaanza kuzitumia kwenye michuano ya Mapinduzi hapa Zanzibar, pia tutazitumia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
“Mashabiki wanaweza kununua jezi zetu mpya kwa ajili ya klabu yao, imekua ni kawaida yetu kufanya jambo hili na wengine wamekua wakituiga…”
Social Plugin