***********
NA EMMANUEL MBATILO
Kwa mara nyingine tena klabu ya Simba Sc imepokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Kagera Sugar kwenye mechi ya ligi kuu NBC mchezo ambao ulipigwa katika dimba la Kaitaba mkoani Kagera.
Licha ya Simba Sc kutawala mchezo huo, hawajabahatika kupata bao kwenye mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake.
Shujaa wa mchezo huo uende kwa Mshambuliaji raia wa Uganda mkongwe Hamisi Kiiza ambaye alipachika bao zuri kipindi cha pili kwenye mchezo huo.
Licha ya kuisadia timu yake kuibuka na ushindi huo, Hamisi Kiiza alipewa kadi nyekundu baada ya kuonesha utovu wa nidhamu.
Social Plugin