Simba SC imeandika historia mpya baada ya kubeba Kombe la Mapinduzi kwa kuitandika Azam FC kwa goli 1-0 katika uwanja wa Amaan, Zanzibar.
*************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Simba wamefanikiwa kunyakua taji la Mapinduzi Cup mara baada ha kuwachapa Azam Fc kwenye mchezo ambao ulihudhuriwa na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi.
Bao pekee la Simba Sc liliwekwa kimyani na Meddie Kagere ambaye alipachika kwa mkwaju wa penati mara baada ya Sakho kuchezewa faulu ndani ya boksi.
Mchezo huo ambao ulikuwa na hisia kwa mashabiki uwanja wa Amani ulijawa na Mashabiki wengi ambao walioshuhudia mtanange huo.
Social Plugin