Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SITA WAKAMATWA TUHUMA ZA KUUA MZEE SERENGETI




JESI la Polisi mkoani Mara linawashikilia watu sita kwa tuhuma za mauaji ya bikizee mkazi wa kijiji cha Rigicha wilayani Serengeti, Wankuru Mwita (88) huku chanzo cha mauaji hayo kikidaiwa kuwa ni imani za kishirikina.

Miongoni mwa watuhumiwa wanaoshikiliwa kuhusiana na tukio hilo lililoteokea Januari 15 mwaka huu ni mke wa mtoto wa marehemu pamoja na waganga wawili wa kienyeji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano, Januari 26, 2022 Kamamda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibushubwamu amesema kuwa watu hao wanatuhumiwa kumuua kwa kumkatakata mapanga mwanamke huyo.

Amesema kuwa kabla ya kufanya tukio hilo watuhumiwa hao walikubaliana kutekeleza mauaji hayo kwa malipo ya Tsh 500,000 wote kwa pamoja na kwamba walipewa Sh50,000 kama kianzio pesa ambazo mke wa mtoto wa marehemu alilipwa kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini (Tasaf) huku wakiahidiwa kumaliziwa kiasi Sh 450,000.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com