Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TCDC SACCOS KUANZISA UWAKALA WA HUDUMA ZA KIFEDHA


Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (TCDC SACCOS) Bw.Aron Ibrahim,akiwasilisha taarifa ya chama iliyoandaliwa na wajumbe wa bodi kwa kushirikiana na watendaji wa chama hicho wakati wa Mkutano wa chama hicho uliofanyika leo Desemba 31,2021 jijini Dodoma.


Mkaguzi kutoka Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) Bi.Dora Meka,akitoa taarifa ya ukaguzi Mkutano wa chama cha Akiba na Mikopo (TCDC SACCOS LTD) kilichofanyika leo Desemba 31,2021 jijini Dodoma.


Wajumbe wakifatilia majadiliano mbalimbali Mkutano wa chama cha Akiba na Mikopo (TCDC SACCOS LTD) kilichofanyika leo Desemba 31,2021 jijini Dodoma.


Mjumbe akiuliza swali wakati wa Mkutano wa chama cha Akiba na Mikopo (TCDC SACCOS LTD) kilichofanyika leo Desemba 31,2021 jijini Dodoma.

*********

Na Alex Sonna, Dodoma

CHAMA cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (TCDC Saccos Limited), kimejipanga kuanzisha miradi mbalimbali ikiwamo uwakala wa huduma za kifedha kwa mitandao ya simu na mabenki ili kuongeza mapato ya chama na kujenga mtaji wa ndani.

Mwenyekiti wa Chama hicho, Aron Ibrahim ameyasema hayo leo kwenye Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika jijini Dodoma.

Amesema Mkutano umeshauri kuwa Bodi ya Uongozi kuomba kibali kwa Mrajis wa Vyama vya Ushirika ili aruhusu kuendesha biashara ya uwakala wa mitandao ya simu pamoja na benki.

Vile vile, Mwenyekiti huyo amesema chama kitaendelea kuhamasisha Watumishi kujiunga na SACCOS hususan wa Mikoani na Wilayani, kuendelea kufuatilia na kutoa hamasa kwa wanachama kumaliza kulipa Hisa na kuendelea kuweka akiba kila mwezi.

Pia amesema TCDC SACCOS itaendelea kushirikiana na Mwajiri kudhibiti wanachama wanaochelewesha marejesho ya mikopo.

Awali, akitoa taarifa ya ukaguzi, Mkaguzi kutoka Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), Dora Meka, amesema hesabu za chama zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha unaoishia Desemba 31, mwaka 2019 kwa kuzingatia viwango vya Ukaguzi.

“Katika ukaguzi wa chama kwa mwaka 2019 chama hakikupata hoja yoyote kwa kuwa hoja zilizojitokeza kwa miaka miwili ya nyuma mwaka 2017 na mwaka 2018 ambapo ilikuwa hoja ya kutumia 'cash basis' badala ya 'accrual basis', kamati ya usimamizi kutotekeleza majukumu yake; hoja hizi zilifanyiwa kazi kipindi cha ukaguzi wa mwaka 2019. Tunaipongeza Bodi ya TCDC SACCOS kwa Usimamizi mzuri,”amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com