Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TCRA YAKIFUNGIA KIPINDI CHA MCHUNGAJI JOSEPHAT MWINGIRA



MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kwa miezi mitatu kipindi cha Efatha Ministry kinachorushwa kupitia kituo cha televisheni cha Star TV, kwa kukiuka kanuni za maudhui ya Utangazaji za mwaka 2018.

Uamuzi huo umetolewa leo Januari 24 ,2022 na Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Abby Gunze.

Kipindi hicho kinachorushwa mubashara na Mchungaji, Josephat Mwingira kilitumia lugha ya matusi dhidi ya mamlaka ya juu ya nchi.

Chanzo- Global publishers

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com