Meneja wa Vivuko vya Magogoni Mhandisi Samwel Chibwana (wa pili kushoto) akikabidhi viti vya watu wenye ulemavu kwa viongozi wa asasi za haki na Usawa kwa Watu wenye Ulemavu (Equal Right for People with Disability Tanzania) ili kupunguza changamoto za usafiri kwa watu wenye ulemavu.Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi ndogo za TEMESA leo Jijini Dar es Salaam. Katibu wa asasi za haki na Usawa kwa Watu wenye Ulemavu (Equal Right for People with Disability Tanzania) Bw.Salmin Hassan akikijaribu kiti cha watu wenye ulemavu mara baada ya kupokea msaada viti hivyo kutoka TEMESA viweze kuwasaidia watu wenye ulemavu wakiwa katika shughuli zao za kila siku.Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi ndogo za TEMESA leo Jijini Dar es Salaam. Meneja wa Vivuko vya Magogoni Mhandisi Samwel Chibwana akizungumza mara baada ya kukabidhi viti vya watu wenye ulamavu kwa Uongozi wa asasi za haki na Usawa kwa Watu wenye Ulemavu (Equal Right for People with Disability Tanzania).Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi ndogo za TEMESA leo Jijini Dar es Salaam. Katibu wa asasi za haki na Usawa kwa Watu wenye Ulemavu (Equal Right for People with Disability Tanzania) Bw.Salmin Hassan akitoa pongezi kwa uongozi wa TEMESA mara baada ya kupokea msaada viti vya watu wenyye ulemavu kutoka TEMESA viweze kuwasaidia watu wenye ulemavu wakiwa katika shughuli zao za kila siku.Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi ndogo za TEMESA leo Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wamekabidhi viti vitano vya watu wenye ulemavu kwa asasi za haki na Usawa kwa Watu wenye Ulemavu ili viweze kusaidia kupunguza changamoto za usafiri kwa watu hao.
Akizungumza katika zoezi hilo lililofanyika katika ofisi ndogo za TAMESA leo Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAMESA, Meneja wa Vivuko vya Magogoni Mhandisi Samwel Chibwana amesema wamekuwa wakiendelea kushirikiana na jamii kuwapa misaada pale bajeti ikiwa inaruhusu kwa mujibu wa mgawio kwa kuwahudumia wale wenye ulemavu katika jamii.
Amesema huduma wanazozitoa zinawagusa watu wenye ulemavu kwani katika huduma wanazozitoa pia husafirisha wananchi hususani katika vivuko kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine, wakati wa utoaji huduma mara nyingi miongoni mwa watu wanaotumia vivuko ni watu wenye ulemavu kwahaiyo wameona watoe msaada wa viti ili viweze kuwasaidia katika huduma za uvukaji na katika safari zao nyingine.
"TEMESA itaendelea kuweka mikakati mbalimbali ikiwezekana kuweka bajeti kila mwaka kwaajili ya kuwasaidia watu wenye ulemavu ili walemavu hao waone na wao hawajatengwa katika huduma hizi zinazotolewa na TEMESA". Amesema Mhandisi Chibwana.
Amesema mbali na misaada hiyo inayotolewa na Serikali lakini pia wana baiskeli kwaajili ya watu wenye ulemavu ambao wanahudumiwa wanapofika kwenye kivuko chochote na baadae kukiacha na kuendelea na safari yake.
Nae Mtunza hazina wa asasi za haki na Usawa kwa Watu wenye Ulemavu (Equal Right for People with Disability Tanzania) Bw.Hilari Ngatunga ameipongeza TEMESA kwa kuwapatia msaada huo ambao utaenda kusaidia watu wenye ulemavu katika shughuli zao za kila siku.
Aidha ameziomba Taasisi zingine mbalimbali zijaribu kuwajali watu wenye ulemavu kwani wamekuwa na uhitaji mkubwa kila siku kwa maana kuna ongezeko kubwa la watu wenye ulemavu.