MAKAMU Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu amesema Kamati Kuu ya Chama chake imeadhimia yeye pamoja na mwanasiasa Godbless Lema kurejea nchini ili kushiriki shughuli za kisiasa na ujenzi wa taifa.
Akizungumza kwa njia ya mtandao jana Ijumaa Disemba,31, Lissu amesema “hatuwezi kuendelea kuishi uhamishoni,” na kwamba yeye na wanasiasa wengine wataanza kufanya maandalizi ya kurejea nchini kati ya Machi na Aprili 2022.
“Huu ni mwanzo wa harakati mpya. Ni mwanzo wa wakimbizi kurudi kujenga nchi yetu,” amesema Lissu nakuongeza kuwa viongozi wa Chadema wataendelea na maandalizi ya kuwapokea wanachama hao na maandalizi yakiwa tayari watatangaza tarehe na muda maalumu wa wao kurejea nchini.
Social Plugin