Na John Walter-Manyara
Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara linawashikila Viongozi watatu wa CHADEMA kwa kosa la kufanya mkutano bila kibali katika eneo la Stendi ya Katesh wilayani Hanang.
Viongozi wanaoshikiliwa ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (BAWACHA) mkoa wa Manyara Regula Mtei (45), Valentina Shayo (37) Mhasibu wa Bawacha mkoa wa Manyara na mjumbe wa Kamati tendaji BAWACHA wakifanya mkutano wa hadhara bila kibali.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Benjamin Kuzaga katika taarifa hiyo ya Januari 19.2022, imeeleza kuwa viongozi hao walifanya kosa hilo Januari 15 mwak huumajira ya saa tisa alasiri wilayani humo.
Taarifa hiyo iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii imeeleza kuwa baada yaviongozi hao kukamatwa na kufikishwa kituoni walihojiwa na kukiri kosa lao na kwamba 17.1.2022 walifikishwa mahakamani.
Social Plugin