Zoezi likiendelea la kuteketeza vipodozi viambata sumu vyenye uzito wa Tani moja na thamani ya millioni 70 ambavyo vilikamatwa katika kaguzi mbalimbali zilizofanywa hivi karibuni na TBS katika mikoa ya kanda hiyo ambayo ni Arusha, Kilimanjaro,Manyara na Tanga. Zoezi likiendelea la kuteketeza vipodozi viambata sumu vyenye uzito wa Tani moja na thamani ya millioni 70 ambavyo vilikamatwa katika kaguzi mbalimbali zilizofanywa hivi karibuni na TBS katika mikoa ya kanda hiyo ambayo ni Arusha, Kilimanjaro,Manyara na Tanga. Mkaguzi wa TBS Kanda ya kaskazini Bw.William Mhina akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuteketeza vipodozi viambata sumu vyenye uzito wa Tani moja na thamani ya millioni 70 ambavyo vilikamatwa katika kaguzi mbalimbali zilizofanywa hivi karibuni na TBS katika mikoa ya kanda hiyo ambayo ni Arusha, Kilimanjaro,Manyara na Tanga.
*******************
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza vipodozi vyenye viambata sumu katika dampo la Muriet jijini Arusha vyenye uzito wa Tani moja na thamani ya millioni 70 ambavyo vilikamatwa katika kaguzi mbalimbali zilizofanywa hivi karibuni na TBS katika mikoa ya kanda hiyo ambayo ni Arusha, Kilimanjaro,Manyara na Tanga.
Akizungumza katika zoezi hilo mapema hii leo, Mkaguzi wa TBS Kanda ya kaskazini Bw.William Mhina amesema katika kuhakikisha kuwa maeneo yanayojihusisha na uuzaji wa vipodozi yanasajiliwa na Shirika yapo salama na yanafaa ni pamoja na ukaguzi wa bidhaa zinazouzwa katika maeneo hayo.
"Ukaguzi uliofanywa na Ofisi ya Kanda imepelekea kukamatwa na kuondolewa sokoni kwa bidhaa za vipodozi zilizopigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu kwani yana viambata sumu ambayo huweza kudhuru afya ya mtumiaji".Amesema.
Aidha amesema bidhaa zilizokamatwa zenye viambata sumu ziko za aina tofauti tofauti na zinatoka nje ya nchi.
Pamoja na hayo amewaasa wananchi kuacha kutumia vipodozi vilivyopigwa marufuku kwani huleta athari kwa nguvu kazi ya Taifa pindi mtu anapoathirika hulazimika kutumia gharama kubwa kujitibu na muda mwingi hupotea na kushindwa kujenga Taifa.
"Kila mtanzania awe mkaguzi wa bidhaa hizi,tunasisitiza ukaguzi uanzie ndani mwetu sisi wote". Amesema
Amesema orodha ya vipodozi vilivyopigwa marufuku inapatikana kwenye tovuti ya Shirika www.tbs.go.tz, pia wanasambaza vipeperushi kwenye maeneo yote yanayojihusisha na uuzaji wa vipodozi, lengo ni kuhakikisha elimu inafika kwa kila mwananchi.
Social Plugin