TAARIFA YA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI
Leo Tarehe 14 Januari 2022, MPC imefanya Mkutano wa Waandishi wa Habari katika Ukumbi Mdogo wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel pamoja na Viongozi wa klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari aliwajulisha Waandishi wa habari juu ya taratibu za mazishi ya Waandishi ambao walipata ajali walipokua na ziara ya kiserikali kuelekea wilayani Ukerewe
Soko alieleza kuwa taratibu za mazishi zilienda vizuri na kuupumzisha miili ya Waandishi wa habari salama
Pia aliwashukru madaktari wa hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa jitihada nzuri za kunusuru maisha ya majeruhi wa ajali kwani ndani ya siku mbili au tatu wataweza kuinuka na kuanza mazoezi hivyo madaktari wanaandaa utaratibu mzuri kwa majeruhi kuhakikisha Hali zao zinazidi kuimarika.
Pia Mwenyekiti wa MPC aliwaeleza Waandishi wa habari kuwa usalama wa Waandishi wa habari ni muhimu hivyo taasisi/ wadau watakaofanya kazi na Waandishi waweke utaratibu mzuri na mikakati maalumu kwa ajili ya kufatilia weledi wa vyombo vya usafiri watakavyotumia
Kama kutakua na tukio linalohitaji Waandishi kuhakikisha wanajipanga siku kabla ya tukio Ili kupata logistics nzuri na kujiepusha na matukio yanayoweza kuzua taharuki
Mwenyekiti wa kamati ya maafa ya MPC Bw Charles Nyamasiriri alizungumza pia katika Mkutano huo juu ya michango ya rambirambi inayoendelea kutolewa na wadau mbalimbali.
Nyamasiriri alisema fedha zote zitakazopatikana zitatumwa kwa familia za marehemu Waandishi wote waliopata ajali.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza alizungumza na Waandishi na kuwashukuru sana kwa ushirikiano waliotoa juu ya kuwastili Waandishi waliopata ajali
Alizungumza kwa kutoa ushirikiano wa kina kwa familia za wafiwa na kusema Bado wanaendelea kuzungumza na familia zao na kuweka baadhi ya mambo katika utaratibu mzuri.
Mhandisi Gabriel aliwakaribisha Sana wanahabari na kutoa Rai yake kuwakaribisha Sana Nyumbani kwenye ofisi yake endapo kutakua na changamoto yoyote ya kitaaluma wasisite kumueleza.
Mratibu
MPC
14.01.2022
Social Plugin