Watu 11 wameripotiwa kufariki nchini Rwanda tangu sikukuu ya Krismasi baada ya kunywa pombe ya kienyeji inayotengezwa kutumia ndizi katika wilaya ya kusini mashariki mwa nchi hiyo ya Bugesera.
Watu wanne zaidi wanaripotiwa kuwa hospitalini kwa matibabu lakini tayari wamepofuka.
Watu watano walikamatwa siku ya Jumatatu kuhusiana na tukio hilo, akiwemo mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe hiyo nchini humo, Ofisi ya Upelelezi ya Rwanda imethibitisha.
Viwango vya juu vya methanoli vilivyopatikana katika moja ya bia hiyo kwa jina Umuneza, vinaweza kuhusishwa na vifo hivyo, kulingana na Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Rwanda.
Kiwanda cha bia kinachojulikana kama Rwandabev kilikuwa kikifanya kazi bila leseni.
Kampeni ya nchi nzima imezinduliwa ili kupambana pombe za kienyeji ambazo hazijaidhinishwa.
Via BBC Swahili
Social Plugin