Watu watatu wamefariki dunia na wengine 11 kujeruhiwa katika ajali basi iliyotokea katika eneo la Panda Mbili wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo chanzo chake amesema ni mwendo kasi.
Naye mkuu wa wilaya ya Kongwa amewatahadharisha wakazi wa wilaya hiyo wanaoishi pembezoni mwa barabara kuu kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi wanapoona ukikwaji wa sheria za barabarani.
Social Plugin