WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dk Dorothy Gwajima,akizungumza katika kikao cha kwanza cha menejimenti kilichokuwa na lengo la kujenga uelewa wa pamoja na kufanya uchambuzi wa walipotoka,walipo na wanapotaka kuelekea kilichofanyika leo Januari 17,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dk Dorothy Gwajima,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati wa kikao cha kwanza cha menejimenti kilichokuwa na lengo la kujenga uelewa wa pamoja na kufanya uchambuzi wa walipotoka,walipo na wanapotaka kuelekea kilichofanyika leo Januari 17,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dk.Zainab Chaula,akimshukuru Waziri wake Dk Dorothy Gwajima,mara baada ya kufungua kikao cha kwanza cha menejimenti kilichokuwa na lengo la kujenga uelewa wa pamoja na kufanya uchambuzi wa walipotoka,walipo na wanapotaka kuelekea kilichofanyika leo Januari 17,2022 jijini Dodoma.
……………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dk Dorothy Gwajima amesema atawaunganisha wananchi na wadau ili kufanya mapitio ya haraka ya Sera mbalimbali ikiwemo ya Maendeleo ya Jamii ili ziendane na wakati wa sasa.
Hayo ameyasema leo Januari 17,2022 jijini Dodoma wakati akizungumza katika kikao cha kwanza cha menejimenti kilichokuwa na lengo la kujenga uelewa wa pamoja na kufanya uchambuzi wa walipotoka,walipo na wanapotaka kuelekea.
Amesema kuwa Serikali inapanga kuwashirikisha wadau kupitia sera, sheria na miongozo ambayo imepitwa na wakati.
Dk.Gwajima amesema kuwa sera nyingi zimepitwa na wakati naa zimekuwa za siku nyingi ambapo maendeleo ya jamii wana sera imepitwa na wakati na ina miaka 25 sasa tangu itungwe.
“Zipo sera nyingi ambazo zimepitwa na wakati kama vile sera ya wanawake inazaidi ya miaka 25, lakini pia sera ya wazee na watoto ambazo zinahitaji kufanyia marekebisho kwa kushirikiana na wadau”amesema
“Kutokana na hali hii wizara itawaunganisha wananchi na wadau wote kuziangalia sera hizo ili haraka ili kupata sera mpya jambo ambalo ni matamanio ya Rais Samia Suluhu Hassan,”amesema Dk.Gwajima
Aidha,amewasisitiza kuzingatia jukumu lao la msingi la kutengeneza miongozo,sera na ufuatiliaji ili ubaguzi wa kijinsia usionekane na kuchukua nafasi katika jamii.
“Ndani ya kuweka mifumo katika maendeleo ya jamii tuangalie na usawa wa kijinsia kwamba sio kweli huyu hawezi kufanya hili kwa sababu ya jinsia yake,tunajua kuna mambo ya kijinsi kama kubeba mimba,kujifungua haya tunajua mwanaume hawezi kuyafanya hivyo basi kwenye majukumu hayo aheshimiwe ili atupatie mtoto mzuri,na akimaliza jukumu hilo la kibaiolojia akaja kwenye majukumu mengine ya pamoja yasitazamwe kwa ubaguzi wa kijinsia,”amesisitiza
Dk.Gwajima amesema kuwa wizara hiyo inaowajibu mkubwa wa kuhakikisha inakuwa kichocheo cha maendeleo kwa jamii na kila mtu ananufaika na fursa zilizopo nchini.
“Ili jamii iendele pia amani na utulivu inahitaji kuwepo hivyo maafisa maendeleo ya jamii wanatakiwa kutimiza wajibu wao kama ambavyo walivyo ajiliwa”amesema Dk. Gwajima
Social Plugin