*************************
NA EMMANUEL MBATILO,
KLABU Yanga imefanikia kusonga mbele hatua inayofuata mara baada ya kufanikiwa kuiondoa Mbao Fc kwa kuwanyuka bao 1-0 katika dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza leo hii.
Bao pekee la Yanga Sc liliwekwa kimyani na Mshambuliaji wao hatari Fiston Mayele ambaye alimalizia krosi iliyopigwa na Farid Mussa na kuweza kupachika bao kwa kichwa kilichoomshinda kipa wa Mbao Fc na kutinga nyavuni.
Kipindi cha kwanza milango yote ilikuwa migumu kwani mechi ilikwendaa mapumziko kwa timu zote mbili zikiwa hazijapata bao.
Kesho mahasimu wao Simba Sc watashuka dimbani kumenyana na Dar City katika dimba la Benjamin Mkapa .
Social Plugin