Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Omar Said Shaaban (Katikati) akitazama maabara ya Shirika la viwango Tanzania (TBS) mara baada ya kutembelea Makao Makuu ya TBS Ubungo Jijini Dar es Salaam akifuatana na baadhi ya Maafisa wa Wizara yake ili kujifunza wakati huu ambao Zanzibar inaimarisha Shirika lake la Viwango ZBS.Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt. Athuman Ngenya.Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Omar Said Shaaban (kushoto) akimsikiliza mmoja wa maafisa viwango wa Shirika la viwango Tanzania (TBS) mara baada ya kutembelea Makao Makuu ya TBS Ubungo Jijini Dar es Salaam akifuatana na baadhi ya Maafisa wa Wizara yake ili kujifunza wakati huu ambao Zanzibar inaimarisha Shirika lake la Viwango ZBS.Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Omar Said Shaaban (Katikati) akiapata picha ya pamoja na watumishi wa Shirika la viwango Tanzania (TBS) mara baada ya kutembelea Makao Makuu ya TBS Ubungo Jijini Dar es Salaam akifuatana na baadhi ya Maafisa wa Wizara yake ili kujifunza wakati huu ambao Zanzibar inaimarisha Shirika lake la Viwango ZBS.Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt. Athuman Ngenya.
**************************
NA EMMANUEL MBATILO,DAR ES SALAAM
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Omar Said Shaaban ameipongeza Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuijengea Shirika la Viwango Tanzania (TBS) uwezo wa kuwa na maabara zenye umahiri wa kutambulika Kimataifa,
Amesema mpaka sasa TBS imekuwa na maendeleo makubwa kwani imeimarisha mifumo ya Tehama pamoja na kufungua ofisi za kikanda kwaajili ya kurahishsa huduma.
Ameyasema hayo leo mara baada ya kutembelea Makao Makuu ya TBS Ubungo Jijini Dar es Salaam akifuatana na baadhi ya Maafisa wa Wizara yake ili kujifunza wakati huu ambao Zanzibar inaimarisha Shirika lake la Viwango ZBS.
"Wakati Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa katika hatua za kuiimarisha ZBS, Taasisi hiyo ambayo bado ni changa, itaendelea kujifunza na kupata uzoefu kutoka TBS, kwa kuwa mashirika haya mawili yana lengo moja la kuhakikisha bidhaa na huduma zinazotumiwa na binadamu zipo salama bila kuathiri afya na mazingira". Amesema Waziri Shaaban.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt. Athuman Ngenya ameahidi kutekeleza maelekezo ya Waziri Shaaban pamoja na kuendeleza ushirikiano na ZBS ili mashirika hayo yaweze kutoa huduma stahiki kwa wananchi kwa ujumla.
Social Plugin