Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC SOPHIA MJEMA AZINDUA RASMI MFUMO WA ANWANI ZA MAKAZI MKOA WA SHINYANGA..AWEKA VIBAO MTAA WA SOKONI NA UHURU ROAD


Uzinduzi wa Mfumo wa Anwani za Makazi mkoa wa Shinyanga ukiendelea  leo Ijumaa Februari 18,2022

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema amezindua Mfumo wa Anwani za Makazi mkoa wa Shinyanga kwa kuweka Vibao vya Maelekezo ya Mtaa wa Barabara ya Uhuru (Uhuru Road) na Sokoni (Market Street) pamoja na Namba za Majengo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika Manispaa ya Shinyanga huku akisisitiza kuwa zoezi hilo linatakiwa likamilike ifikapo mwezi Aprili 2022 katika mitaa yote mkoani Shinyanga.

Uzinduzi wa Mfumo wa Anwani za Makazi unaohusisha uwekaji mabango (vibao) ya maelezo ya mtaa, uwekaji namba kwenye nyumba na taarifa za ndani ya nyumba umefanyika leo Ijumaa Februari 18,2022 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ngazi ya Mkoa na Halmashauri zote sita za mkoa wa Shinyanga likishuhudiwa na wananchi Mjini Shinyanga. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Mjema amesema uzinduzi wa Mtaa wa Sokoni katika Manispaa ya Shinyanga unawakilisha mitaa yote katika mkoa wa Shinyanga akibainisha kuwa mfumo wa Anuani za Makazi utasaidia kuwatambua wananchi hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali katika jamii.

“Zoezi hili la kutambua makazi linatakiwa likamilike hadi ifikapo mwezi Aprili mwaka huu. Anuani za Makazi utasaidia kuwahudumia wananchi kwa ufanisi. Mwaka huu zoezi la Sensa litafanyika kikamilifu kwani itakuwa ni Sensa ya Watu na Makazi. Hii itakuwa tofauti na miaka ya nyuma kidogo ambapo tumekuwa na Sensa ya watu pekee bila makazi yao. Anuani za Makazi zitarahisisha zoezi hili kwani Sensa itahusisha kujua idadi ya wakazi, nyumba zao na kutambua mitaa yao”,amesema Mjema.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amewataka wananchi kutunza alama hizo za utambuzi wa makazi kwani zitasaidia kurahisisha kutambua mitaa na nyumba za wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (katikati aliyevaa kiremba) baada ya kuzindua rasmi Mfumo wa Anwani za Makazi mkoa wa Shinyanga kwa kuweka Vibao vya Maelekezo ya Mtaa wa Sokoni "Market Street" na Barabara ya Uhuru "Uhuru Road" katika Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa Maandishi ya upande wa pili wa Vibao vya Maelekezo ya Mtaa wa Sokoni "Market Street" na Barabara ya Uhuru "Uhuru Road" katika Manispaa ya Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akizindua rasmi Mfumo wa Anwani za Makazi mkoa wa Shinyanga  leo Ijumaa Februari 18,2022. 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akizindua rasmi Mfumo wa Anwani za Makazi mkoa wa Shinyanga  leo Ijumaa Februari 18,2022. 
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akizindua rasmi Mfumo wa Anwani za Makazi mkoa wa Shinyanga  leo Ijumaa Februari 18,2022. 
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akizindua rasmi Mfumo wa Anwani za Makazi mkoa wa Shinyanga  leo Ijumaa Februari 18,2022. 
Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Ibrahim Kiyungu akizungumza baada ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kuzindua Namba 28 ya Jengo la TANESCO  wakati akizindua rasmi Mfumo wa Anwani za Makazi mkoa wa Shinyanga  leo Ijumaa Februari 18,2022. 
Namba 28 ya Jengo la TANESCO  
Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga Pendolake Msangi akizungumza baada ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kuzindua Namba 32 ya Jengo la TANESCO  wakati akizindua rasmi Mfumo wa Anwani za Makazi mkoa wa Shinyanga  leo Ijumaa Februari 18,2022. 
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza baada ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kuzindua rasmi Mfumo wa Anwani za Makazi mkoa wa Shinyanga  leo Ijumaa Februari 18,2022. 

Picha na Kadama Malunde - Malunde  1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com