Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HALMASHAURI YA SHINYANGA YAPOKEA SH. MILIONI 900 KUPANGA, KUPIMA NA KULIPA FIDIA VIWANJA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy akizungumza wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika leo Jumatano Februari 23,2022.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imeomba na kufanikiwa kukopeshwa na Serikali kuu jumla ya shilingi Milioni 900 kwa ajili ya kugharamia kupanga, kupima na kuthaminisha/kulipa fidia ya viwanja vya matumizi mbalimbali katika Miji ya Mwakitolyo, Solwa, Salawe, Iselamagazi, Ishinabulandi, Busanda, Tinde, Puni na Didia.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy wakati akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Kupanga, Kupima na Kukamilisha Ardhi wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika leo Jumatano Februari 23,2022. 

Munissy ameeleza kuwa Mpango huo unalenga kuwepo kwa ardhi iliyopangwa, kupimwa na yenye usalama wa miliki pamoja na kuinua thamani ya ardhi, kupunguza migogoro ya ardhi, kuzitumia hatimiliki za ardhi kama mtaji wa kuwainua kiuchumi wananchi/wamiliki, kuiingizia mapato serikali kutokana na kodi/tozo mbalimbali za ardhi na maendelezo yake na kuwepo kwa miji/makazi yenye mandhari nzuri.

“Mpango huu unatekelezwa kwa awamu katika Miji ya Mwakitolyo, Solwa, Salawe, Iselamagazi, Ishinabulandi, Busanda, Tinde, Puni na Didia. Maeneo haya yametambuliwa na kukubalika kwa kuzingatia sifa za maendeleo kiuchumi,kibiashara na kijamii.Awamu ya kwanza inahusisha Miji ya Solwa, Iselamagazi na Ishinabulandi”,amesema Munissy.

 “Jumla ya shilingi Milioni 900 za utekelezaji wa mpango ambazo zimepokelewa mwezi Januari 2022 zitatumika katika kupanga na kupima viwanja,kufanya uthamini na kulipa fidia ya ardhi na maendelezo yake,usimamizi wa mpango na kumilikisha viwanja na kufungua barabara kuu maeneo ya mpango”,ameongeza Munissy.

“Tayari tumeshapima viwanja 2000 ikiwa ni juu ya makadirio ya viwanja 1500 tulivyoombea shilingi milioni 900 na taratibu za mauzo ya viwanja  zimeanza na vinatarajiwa kuanza kuuzwa kuanzia Machi 1,2022",amesema Munissy.

Amefafanua kuwa Viwanja vitakavyopimwa vya makazi  bei ya kila kiwanja makadirio ya sasa ni shilingi 800,000/= viwanja vya makazi/biashara ni  shilingi 1,000,000/=, Taasisi shilingi 6,000,000/=, na viwanda kila kiwanja shilingi 8,000,000/= lakini bei rasmi zitatangazwa Mwezi Machi,2022.

Amesema viwanja vitakavyopangwa na kupimwa na wananchi kutakiwa kuchangia gharama za kupanga na kupima na Wananchi wataruhusiwa kuendeleza au kuuza viwanja vyao baada ya kulipia gharama za upangaji na upimaji ardhi ambapo kila kiwanja kimoja cha kawaida cha makazi kitalipiwa shilingi 130,000/=.

“Menejimenti inatarajia kuwa mpango huu utachochea maendeleo ya wananchi, Halmashauri ya wilaya na Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla na kwamba mwenendo wa utekelezaji wa mpango upo ndani ya Mpango kazi na menejimenti ina matumaini ya kukamilisha utekelezaji wa mpango ndani ya wakati”,amesema.

Hata hivyo amesema Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga imeendelea kuomba fedha kutoka Serikalini, wadau wa maendeleo na kuweka kwenye bajeti yake maksio ya fedha kwa ajili ya kupanua wigo wa mpango huo katika maeneo mengine.

ANGALIA PICHA HAPA
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Kupanga, Kupima na Kukamilisha Ardhi wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika leo Jumatano Februari 23,2022.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika leo Jumatano Februari 23,2022.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngasa Mboje akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika leo Jumatano Februari 23,2022.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngasa Mboje akiongoza  kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika leo Jumatano Februari 23,2022.

 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Isack Sengelema akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiendelea na kikao 

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava akiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela (kushoto) na Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Ernestina Richard wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Wageni waalikwa na Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Wageni waalikwa na Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Soma pia :

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com