****
Na Dinna Maningo - Mara
Akizungumza na Malunde 1 blog ofisi ya UVCCM wilayani hapo Godfrey amesema kuwa UVCCM katika uchaguzi wa 2020 kata 29 kati ya 34 katika wilaya hiyo zinaongozwa na madiwani vijana.
Amesema kuwa katika halmashauri ya wilaya ya Tarime, vijiji 55 kati ya vijiji 88 vinaongozwa na wenyeviti wa vijiji ambao ni vijana huku katika halmashauri ya mji Tarime yenye mitaa 81 kati ya hiyo mitaa 25 inaongozwa na wenyeviti vijana.
"Miaka ya nyuma vijana waliojitokeza kugombea uongozi katika siasa walikuwa wachache ila kwa sasa vijana wamekuwa wakijitokeza kugombea,Jumuiya yetu ya Vijana Madiwani na wenyeviti wa mitaa na vijiji wengi ni vijana"amesema Godfrey.
Ameongeza kuwa katika ajira vijana 15 kutoka UVCCM wameajiliwa serikalini katika kipindi cha mwaka 2017-2022 nakwamba hali hiyo imechochea vijana kuzidi kukipenda chama.
Akizungumzia mafanikio ya miradi ya UVCCM, amesema kuwa Jumuiya hiyo ina maduka matatu kama kitega uchumi,imeanzisha ujenzi wa nyumba ya kuishi ya katibu wa UVCCM ujenzi uliofikia hatua ya msingi lakini pia kusimamia na kufatilia ujenzi wa miradi ya maendeleo inayojengwa na serikali.
" Tuna mkakati wa kuwa na mradi wa Usafirishaji ambapo tunatarajia kununua gari mbili aina ya Basi kwa ajili ya kusafirisha abiria na tuna mpango wa kuwa na kiwanda cha kufyatua matofari"amesema.
Mwenyekiti huo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suhuhu kwa kuendelea kuteuwa vijana katika nafasi mbalimbali za uongozi huku akipongeza mikopo inayotolewa kwa vijana, kwakuwa imewezesha vikundi 115 vya vijana walio wanachama na wasio wanachama kupata mikopo isiyo na riba ambayo imeinua biashara zao.
Ghati Mkami mkazi wa mtaa wa Nyandoto anakipongeza chama cha Mapinduzi kwa kuwajali vijana na kuwapatia fursa mbalimbali ambazo zimewawezesha kujiinua kiuchumi tofauti na miaka ya nyuma vijana walikuwa na nafasi ndogo kupewa kipaumbele katika nafasi za uongozi.
Yusuph Nyamhanga mkazi wa Mtaa wa Mwangaza anasema kuwa UVCCM Tarime imekuwa ikipokea changamoto kutoka kwa wananchi na wamekuwa mstari wa mbele kusaidia kutatua kero za vijana hususani waendesha pikipiki (Bodaboda).
Social Plugin