SHIRIKA LA IYMT LATOA MAFUNZO YA UVIKO - 19 KWA WADAU SHINYANGA

Washiriki wa semina maalumu kuhusu Uviko - 19 na HIV iliyoandaliwa na shirika la IYMT wakipiga picha ya pamoja.

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Shirika lisilo la kiserkali linalojishughulisha na Uwezeshaji Kiuchumi na masuala ya kiafya kwa Vijana la Igniting Young Minds Tanzania (IYMT) kwa ufadhili wa Amref Tanzania limekutana na wadau mbalimbali wa kupambana na Uviko - 19 mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kujadili matokeo ya uwepo wa ugonjwa wa Uviko 19 katika jamii sanjari na kujua namna ambavyo jamii inaendelea kupambana na ugonjwa huo.

Semina hiyo maalumu kuhusu Uviko - 19 na HIV imefanyika leo Jumatano Februari 2,2022 katika Ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga.

Mkurugenzi wa shirika la IYMT Michael Maganga amesema lengo la semina hiyo ni kufahamu ni namna gani jamii inaendelea kujikinga na kuchukua tahadhari za ugonjwa wa Uviko 19.

“Madhumuni yetu ni kufahamu ni namna gani jamii inaendelea kujikinga na kuchukua tahadhari za ugonjwa wa uviko 19 ikwemo kuvaa barakoa,kutumia vitakasa mikono, lakini pia kupata takwimu za uchanjaji chanjo kwa wananchi zipoje na jamii imepokeaje chanjo ili tujue ni namna gani tunawezaa kusaidia na kushirikiana na wadau kuhakikisha jamii wanapata taarifa sahihi dhidi ya Uviko 19”, amesema Maganga.

“Lakini pia kusaidia na kuwaandaa watu kutoka sekta mbalimbali ili kuwasaidia wanajamii wanaokutana nao kuwapatia elimu sahihi ya Uviko 19 hususani chanjo”,ameongeza.

Kwa upande wake, Mwezeshaji katika semina, hiyo Dkt. Boniphace Kisalwa kutoka hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga amesema jamii inatakiwa kupatiwa elimu zaidi juu ya uchanjaji wa chanjo za Uviko - 19 kutokana na kuenea kwa elimu isiyokuwa sahihi juu ya chanjo za Uviko- 19 kwa wanajamii hususani kwa watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi ya UKIMWI.

“Taarifa zinakuwa ni nyingi na mapokeo ni tofauti lakini pamoja na hayo tunahamasisha saana uchanjaji kwa watu wote lakini kundi ambalo tunalitilia mkazo ni la watu wanaoishi na maambukizi ya vurusi vya UKIMWI kwani kinga zao za mwili zinakuwa zipo chini hivyo wakichanjwa inasaidia kujiwekea ulinzi hata wakipata maambukizi hawatafika katika hatua za hatari zaidi”, amesema Dkt. Kisalwa.

Naye Afisa Maendeleo ya jamii Manispaa ya Shinyanga na mratibu wa shughuli za Ukimwi Salome Komba amesema mafunzo hayo yataongeza wigo wa utoaji elimu kwa jamii ili kuondoa mitazamo hasi juu ya chanjo ya Uviko- 19.

“Kwenye kutoa elimu kuna watu kazi yao ni kupotosha hivyo tunaendelea kushirikiana kuhamasisha jamii kwamba chanjo haina madhara yeyote ni salama na tunatumia wazee maarufu, viongozi wa sungusungu kwasababu kwenye jamii zetu wakiongea watu maarufu jamii inawaamini zaidi”,ameeleza Komba

Mwezeshaji katika semina maalumu kuhusu Uviko - 19 na HIV iliyoandaliwa na shirika la IYMT , Dkt. Boniphace Kisalwa kutoka hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga akitoa mada kuhusu UVIKO 19

Afisa Mipango wa Shirika la IYMT Cairo Kisanga akizungumza wakati wa semina maalumu kuhusu Uviko - 19 na HIV iliyoandaliwa na shirika la IYMT
Afisa Mipango wa Shirika la IYMT Cairo Kisanga akizungumza wakati wa semina maalumu kuhusu Uviko - 19 na HIV iliyoandaliwa na shirika la IYMT
Mkurugenzi wa shirika la IYMT Michael Maganga akizungumza wakati wa semina hiyo
Meneja wa Mradi wa shirika la IYMT Violet Yongo akiwa ukumbini
Afisa Maendeleo ya jamii Manispaa ya Shinyanga na mratibu wa shughuli za Ukimwi Salome Komba (kulia) akiwa ukumbini.
Sehemu ya washiriki wa semina maalumu kuhusu Uviko - 19 na HIV iliyoandaliwa na shirika la IYMT wakiwa ukumbini
Washiriki wa semina maalumu kuhusu Uviko - 19 na HIV iliyoandaliwa na shirika la IYMT wakipiga picha ya pamoja.
Washiriki wa semina maalumu kuhusu Uviko - 19 na HIV iliyoandaliwa na shirika la IYMT wakipiga picha ya pamoja.

Picha zote na Mpiga picha - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم