POLISI katika jimbo la Bhubaneshwar nchini India wamemkamata Ramesh Chandra Swain anayedaiwa kuwalaghai wanawake 17 kwa kujifanya daktari na wakati mwingine hata Ofisa mkuu wa afya.
Remesh mwenye umri wa miaka 66 anatuhumiwa kuoa kwa njia ya ulaghai wanawake 17 kutoka majimbo nane na kuwaibia pesa, alikamatwa Jumapili usiku katika nyumba moja eneo la Khandagiri huko Bhubaneswar.
Mkuu wa polisi wa jimbo hilo, Bhubaneshwar, amesema kwamba huenda mwanaume huyo aliwalaghai wanawake wengine kando na wanawake hao 17.
Mkuu wa polisi wa jimbo hilo, Bhubaneshwar, aliiambia BBC kwamba huenda mwanaume huyo aliwalaghai wanawake wengine kando na wanawake hao 17 “Tumepokea taarifa kuhusu wanawake watatu kati ya 17 baada ya kukamatwa kwa Ramesh.
Akitoa taarifa za namna Ramesh alivyokamatwa, kamanda huyo alisema “Tumekuwa tukimtafuta mtu huyu kwa siku kadhaa, tumechukua kila hatua kumkamata. “Lakini aliishi Bhubaneswar hivyo kwa muda fulani haikuwezekana kumkamata.
Hatimaye siku ya Jumapili tulipata taarifa kwamba alikuwa amefika Bhubaneshwar na tukamkamata usiku huohuo nyumbani kwake Khandagiri.” Alisema Umashankar Das, gavana wa mkoa.
Social Plugin