Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AMTEKA NA KUMUUA MTOTO WAKE , AJIUA NA KUACHA HELA YA VOCHA



Mwanaume mmoja nchini Kenya aliyefahamika kwa jina la Victor Aliyeko amemteka na kumuua mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu na kisha yeye mwenyewe kujiua, tukio hilo limetokea Nakuru jijini Nairobi.

Inaelezwa Aliyeko aliingia kwa siri nyumbani kwa mke wake wa zamani, wakati alipokuwa kazini na mumewe na kisha kumteka mtoto huyo.

Wakati mama wa mtoto huyo na mumewe, Christopher Okeyo waliporejea nyumbani hawakumkuta mtoto na walikuja kufahamu kuwa baba wa mtoto amemchukua na kuondoka naye.

Wawili hao baada ya kupata taarifa hizo waliamua kwenda nyumbani kwa Aliyeko na kumkuta mtoto wake akining’inia kwenye waya wa umeme na baba yake akiwa kitandani tayari amekwishafariki huku mezani kukiwa na Shilingi za Kenya 500 na ujumbe uliowataka kutumia fedha hizo kununua vocha ili watoe tarifa za kifo chake kwa ndugu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com