JESHI la Polisi Mkoani Arusha linamshikilia kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Raymond Mollel ammbaya amekamatwa kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa mlinzi wa shule ya Winnings Spirit iliyopo eneo la Terati jijini Arusha, Issa Dinaiah (57) aliyekutwa ameuawa kwa kuchinjwa huku kichwa chake kikiwa hakipo.
Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Joshua Mwafrango amekiri kukamatwa kwa kumtuhumiwa huyo ambaye mpaka sasa anaendelea kuhojiwa.
“Tumemkamata kijana mmoja anayeitwa Raymond Mollel kwa tuhuma za mauaji hayo. Huyu mtuhumiwa ni mlinzi mwenzake. Raymond na marehemu walikuwa walinzi wa Meya wa Arusha, Maxmillian Iranghe.
“Baada ya kumkamata tulimhoji, amekiri kutekeleza mauaji hayo na kuonesha alipokificha kichwa cha mwenzake. Pia, kichwa cha marehemu kimepatikana. Hakuna kitu kilichovunjwa wala kuibiwa eneo la tukio, bali ni hayo mauaji yaliyofanyika.
Mwili wa mlinzi huyo ulikutwa jana Jumatano Februari 2, 2022 asubuhi na wafanyakazi wa shule hiyo inayomilikiwa na Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranghe.
Social Plugin