WAZIRI MKUU AAGIZA MAAFISA WA POLISI MTWARA, KILINDI KUSIMAMISHWA KAZI SAKATA LA MAUAJI




Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro awasimamishe kazi maafisa wa Polisi wa Mikoa ya kipolisi ya Mtwara na Kilindi wakiwemo RPC na RCO ili kupisha uchunguzi wa mauaji yaliyotokea maeneo hayo.

 Timu hiyo itafanya kazi kwa siku 14 kuanzia kesho Jumamosi Februari 5,2022.

Hatua hiyo imekuja kufuati agizo la Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutoa agizo la kuundwa tume huru tofauti na tume iliyoundwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Maagizo haya yanakuja kufuatia kifo cha mfanyabiashara wa madini aliyekuwa na umri wa miaka 25, Musa Hamisi mkazi wa wilaya ya Nachingwea mkoa jirani wa Lindi, ambaye anadaiwa kukamatwa na askari wa polisi Oktoba 20, mwaka jana akiwa katika nyumba ya kulala wageni Mkoani Mtwara akituhumiwa kuwa mwizi wa pikipiki na kufikishwa kituo cha poilisi kwa ajili ya mahojiano.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم