Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza wametakiwa kuimarisha mahusiano, ushirikiano na uadilifu baina yao na Wataalamu pamoja na Watendaji mbalimbali wa Halmashauri hiyo ili kwa pamoja kutekeleza vyema maamuzi na maelekezo wanayoyapitisha.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza anayeshughulikia Serikali za Mitaa, Christian Bigambo wakati akifungua semina kwa madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza yenye lengo la kuwajengea uwezo ili kuimarisha uadilifu katika utendaji wao wa kazi.
Bigambo amesema maamuzi na maelekezi mengi yanayotolewa na madiwani yanatekekelezwa na wataalamu pamoja na watendaji mbalimbali hivyo ikiwa kwa pamoja wataimarisha mahusiano, ushirikiano na mahusiano itasaidia utekelezaji wa maamuzi na maelekezo hayo.
Aidha amewataka madiwani hao kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali ya Serikali katika kutekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na zile zinazotolewa na Halmashauri wakati wa kuendesha vikao na kwamba inapotokea mkanganyiko wa kisheria ni vyema wakakaa meza moja na wataalamu na watendaji ili kufikia mwafaka badala ya kuwa na malumbano yasiyo na tija.
Bigambo amewahimiza kusimamia vyema utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kufuatilia mikopo inayotolewa na Halmashauri kwa vikundi vya akina mama, vijana na watu wenye ulemavu ili kuhakikisha vinarejesha mikopo hiyo. Awakumbusha pia kufuatilia matumizi ya fedha za Serikali katika miradi mbalimbali kwa lengo la kujiridhisha kama yanafuata bajeti iliyoidhinishwa hatua itakayosaidia Halmashauri kutopata hati chafu kutoka kwa CAG.
Kwa upande wa kufanya maamuzi mbalimbali ikiwemo kuwachukulia hatua watumishi wasio na nidhamu, Bigambo amewataka madiwani hayo kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu wakati wa kufanya maamuzi hayo hatua itakayosaidia kuondoa dhana ya kuwaonea watumishi.
Naye Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Rodrick Ngoye amesema semina hiyo ni muhimu na itawasaidia madiwani kutekeleza vyema majukumu yao na kwamba watazingatia maelekezo yaliyotolewa wakati wa ufunguzi wa semina hiyo pamoja na yale watakayojifunza kupitia mada mbalimbali zitakazowasilisha na hivyo kuleta matokeo chanya kwa Halmashauri.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza anayeshughulikia Serikali za Mitaa, Christian Bigambo akizungumza wakati anafungua semina kwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza yenye lengo la kuwajengea uelewa ili kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia weledi na uadilifu.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza anayeshughulikia Serikali za Mitaa, Christian Bigambo (kulia) akifungua semina hiyo. Kushoto ni Naibu Meya Halmashauri ya Jiji la Mwanza Rodrick Ngoye na katikati ni Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mkoa Mwanza, Godson Kweka.
Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza (kushoto) wakimsikiliza Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza anayeshughulikia Serikali za Mitaa, Christian Bigambo (kulia) wakati akifungua semina hiyo.
Naibu Meya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Rodrick Ngoye akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza anayeshughulikia Serikali za Mitaa, Christian Bigambo (katikati) kufungua semina hiyo. Kulia ni Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mkoa Mwanza, Godson Kweka.
Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mkoa Mwanza, Godson Kweka akiwasilisha mada kuhusu Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza (hawako pichani).
Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza (kulia) wakimsikiliza Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mkoa Mwanza, Godson Kweka (kushoto) wakati akiwasilisha mada kwenye semina hiyo.
Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mkoa Mwanza, Godson Kweka (kushoto) akiwasilisha mada kwenye semina hiyo.
Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mkoa Mwanza, Godson Kweka akiwasilisha mada kwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Semina hiyo ya siku mbili inalenga kuwajengea uwezo/ uelewa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ili kutekeleza kwa uailifu majukumu yao.
Semina hiyo imewashirikisha Madiwani kutoka Kata 18 za Halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na Madiwani wa Viti Maalum ambapo kwa pamoja wamehimizwa kufanya kazi kwa ushirikiano na uadilifu ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza anayeshughulikia Serikali za Mitaa, Christian Bigambo (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza (waliosimama) baada ya kufungua semina ya kuwajengea uwezo ili kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia Maadili ya Viongozi wa Umma. Wengine waliokaa ni Naibu Meya Halmashauri ya Jiji la Mwanza Rodrick Ngoye (kushoto) na Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mkoa Mwanza Godson Kweka.

SOMA>>> Habari zaidi hapa