Joan Burke
Kwa mujibu wa polisi kutoka kituo Palm Springs, walisema kwamba walipokea simu mnamo Februari 11, 2022, kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kama ni mtoto wa mtuhumiwa baada ya kufika nyumbani na kukuta mwili wa baba yake wa kambo Melvin Weller (62) ukiwa chini na umezungukwa na damu nyingi, na ndipo maafisa wa polisi walipofika eneo la tukio.
Kufuatia uchunguzi wa madaktari uliofanywa kwenye mwili wa mwanaume huyo ulibaini kwamba alipata zaidi ya majeraha 140 ya kuchomwa na kuvunjika kwa fuvu la kichwa baada ya kupigwa na kisu cha nyama.
Chanzo : BBC Swahili
Social Plugin