Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru akishirikiana na mwananchi wa kata ya Chang'ombe kupanda mti ili kuhifadhi mazingira
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru akishirikiana na mwananchi wa kata ya Chang'ombe kupanda mti ili kuhifadhi mazingira
*****
Na Dotto Kwilasa-Malunde 1 Blog-DODOMA.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM)kikiwa kimetimiza miaka 45 tangu kuanzishwa kwake, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru ametumia kuienzi siku hiyo kwa kuwaongoza wakazi wa kata ya Chang'ombe Jijini hapa kufanya usafi na kupanda miti huku akipiga marufuku wananchi kufanya shughuli za kibinadamu zinazo athiri mazingira.
Hayo yamejiri leo jijini Dodoma katika Kata ya Chan'gombe ambapo amesema wanafanya vitu viwili kwa wakati mmoja ambavyo ni usafi wa mazingira na kupanda miti ili kustawisha Jiji hilo.
Amesema kila mwananchi anapaswa kutii sheria za mazingira ili kupendezesha Jiji la Dodoma na kwamba Kwa kufanya hivyo Jiji litakuwa na hali ya usafi ambao utasaidia watu kuishi bila hofu ya maradhi.
Kwa upande wake,Afisa Mazingira wa Jiji la Dodoma,Dickson Kimaro amesema wamekuwa wakiendelea na zoezi la utoaji wa elimu kuhusu uzoaji wa taka ambapo kaya nyingi zimekuwa zikijitokeza kufanya usafi.
"Kupitia mgambo wa jiji la Dodoma tutahakikisha sheria za uhifadhi wa mazingira zinafutwa,kwa wale wakaidi tutawatoza faini ya shilingi 50000 hadi 300000 ,"amesema