NDEGE INAYOTUMIA UMEME KUANZA MAJARIBIO, HAITUMII MAFUTA




TEKNOLOJIA na masuala ya usafirishaji inazidi kuwa kubwa, wakati wengine wakibuni magari mapya yanayotumia umeme badala ya mafuta, Israel Eviation wamekuja na kitu cha tofauti.

Kampuni ya Israel Eviation imetengeneza ndege ya kwanza ya abiria duniani ambayo inatumia umeme kwa asilimia 100 bila mafuta hata tone, ambayo imefanyiwa majaribio ya awqali wiki iliyopita huko Arlington Municipal Airport, Kaskazini mwa Seattle huko Washington nchini Marekani.


Ndege hiyo ya Alice sasa imebakiza wiki chache ili kufanya safari yake ya kwanza tangu itengenezwe ikiwa na uwezo wa kubeba Abiria 9 na marubani wawili na kuruka kwa 250 kts, au maili 287 287 kwa saa. Ikumbukwe kuwa ndege aina ya Boeing 737 ina mwendokasi wa maili 588 kwa saa.

Kampuni hiyo iliyomtengeneza Alice ambayo imejikita katika usafiri wa anga kwa teknolojia ya umeme, inaamini kwamba ndege zinazotumia umeme zenye uwezo wa kubeba Abiria 20 mpaka 40 zitakuwa sokoni ndani ya miaka 7 hadi 10 ijayo (mwaka 2029 – 2032).


Ndege hiyo iliyoanza kutengenezwa mwaka 2019 imepitia katika mabadiliko ya aina mbalimbali na majaribio kadhaa ikiwemo majaribio la mwendokasi kuanzia speed ya chini mpaka speed kubwa ambapo majaribio mengine yalifanyika Desemba, mwaka jana.

Alice sasa itafanyiwa majaribio mengine ya speed tofauti tofauti, umeme wake ambapo inatumia betri na uwezo wake, mifumo ya steering, brak, na uratibu wa masafa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post