Na Dinna Maningo, Musoma
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa,ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Jicho la Chama litakuwa karibu kufuatilia wanachama walioanza mapema pilikapilika za kampeni katika mkoa wa Mara.
Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa ameyasema hayo Leo Februari 5,2022 wakati wa kilele cha maadhimisho ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa chama hicho Februari 5,1977,sherehe zilizoambatana na burudani mbalimbali na uzinduzi wa kadi mpya za wanachama za mfumo wa kielektroniki.
"Tumeanza kuona pilikapilika hapa Mara za kampeni tunafuatilia,kila mtu ana haki ya kugombea,jicho la chama litakuwa karibu kufatilia" ,amesema Samia.
Ameongeza kuwa mwaka huu 2022 ni uchaguzi ndani ya chama hicho na kwamba wanatakiwa viongozi imara ili kufanikisha vyema kwenye uchaguzi,amewahimiza viongozi na Jumuiya zake kufanya kazi kwa bidii.
Amesema kuwa safari ya miaka 45 haikuwa nyepesi kwasababu kulikuwa na ushindani na vyama vingine nakwamba ushindi wa CCM umetokana na chama hicho kujenga imani na hivyo kuaminiwa na wananchi.
TAZAMA <<HAPA>> PICHA SHEREHE ZA MIAKA 45 YA CCM 2022