Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SIMBA SC WAFANYA MAUAJI YA KUTISHA... WAIFYATUA RUVU SHOOTING 7-0, CHAMA BALAA


Na Emmanuel Mbatilo - Dar es salaam

KLABU ya Simba imefanya kufuru kwa kufanikiwa kuinyuka timu ya Ruvu Shooting kwa mabao 7-0 kwenye mchezo wa kombe la Azam Sport Federation Cup (ASFC) mechi iliyopigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jjijini Dar es Salaam.

Clatous Chama au muite Tripple C ambaye alikuwa mwiba kwenye mechi hiyo mara baada ya kupiga mabao matatu (Hat Trick) na kuiwezesha timu yake kuondoka na ushindi wa mabao 7-0.

Dakika ya kwanza tu ya mchezo iliwafanya Simba Sc kupata bao la mapema la kuongoza kupitia kwa kwa mshambuliaji wao John Bocco ambaye pia kwenye mchezo huo aliweza kupachika mabao mawili ambapo bao lingine alilifunga dakika ya 39 ya mcezo.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizka Simba Sc alikuwa mbele kwa mabao 5-0 ambapo mlima ulikuwa mkubwa kwa Ruvu Shooting kufanya uwezekano wa kurudisha mabao hayo.

Mabao mengine yaliwekwa kimyani na Jimmyson Mwanuke dakika ya 70, Clatous Chama dakika ya 25,27,72 na bapo lingine Ruvu Shooting wakijifunga kupitia kwa Michael Masinda.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com