Wizara ya ulinzi ya Kyiv inadai kuwa takribani wanajeshi 5,300 wa Urusi wameuawa katika siku nne za kwanza za mapigano nchini Ukraine.
Katika taarifa iliyotumwa kwenye Facebook, maofisa wa Ukraine wamedai kuwa mbali na wanajeshi hao, vifaru 191, ndege za kivita 29, helikopta 29 na shehena 816 za kivita zimeharibiwa na vikosi vya Ukraine.
Madai hayo yanafuatia kukiri kwa wizara ya ulinzi ya Urusi siku ya Jumapili kwamba vikosi vyake vimepata hasara, ingawa maofisa hawakutoa takwimu kamili.
Wakati huo huo, waangalizi wa Umoja wa Mataifa walisema wamethibitisha vifo vya raia wasiopungua 94 katika siku za kwanza za mapigano.
Social Plugin