WALIOIBA BILIONI 2 WAKAMATWA IRINGA


Jeshi la Polisi Mkoani Iringa linafanya Uchunguzi/Upelelezi dhidi ya Watuhumiwa wa wizi wa fedha za kitanzania kiasi cha TSh 2,129,856,000 mali ya kampuni ya SELCOM PAYTECH LIMITED.

“Wakala wa Selcom aitwaye Tyson Kasisi wa Iringa kupitia huduma ya ‘Selcom Pay’ isivyo halali alihamisha fedha kwenda namba mbalimbali za simu na kisha kuchukuliwa taslimu kupitia wakala wa huduma za kifedha za mitandao mbalimbali ya simu pamoja na akaunti za Benki”


“Wizi wa fedha hizo ulifanyika kwa njia ya mtandao katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Iringa, DSM na Morogoro kati ya tarehe 9 hadi 27 Novemba, 2021 baada ya wakala huyo Kasisi kufanikiwa kuchezea mfumo wa kieletroniki wa ‘Selcom Pay’ unaomilikiwa na Kampuni ya SELCOM PAYTECH LTD”

“Wakala huyo kwa njia ya udanganyifu alianza kujitumia fedha pamoja na kuwatumia Watu wengine na kwa kushirikiana na genge lake la uhalifu walifanikiwa kuiba kiasi hicho, Jeshi la Polisi Iringa limefanikiwa kukamata (Kuokoa) fedha taslimu kiasi cha TSh 956,974,000 kutoka kwa Watuhumiwa na washiriki wa uhalifu huo ambao walipokea sehemu ya fedha hizo kwa ajili ya kuzificha katika maeneo mbalimbali ikiwemo makazi na shambani.”



“Kiasi cha fedha za kitanzania TSh 121,215,783 zimezuiliwa katika moja ya Benki za biashara mkoani Iringa ikiwa ni mazalia ya uhalifu.”




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post