Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza linamshikilia Dianna Edward Bundala (Zumaridi) mwenye umri wa miaka 39, mkazi wa mtaa wa Buguku kata ya Buhongwa kwa kosa la usafirishaji haramu wa binadamu wapatao 149.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng'anzi amesema watu hao wametolewa na kusafirishwa kutoka sehemu mbalimbali kisha kuwafungia nyumbani kwake ambapo alikuwa akiwatumikisha, kati yao wanaume ni 57, wanawake 92, na miongoni mwao wapo watoto 24 wanaokadiriwa kuwa na miaka kati ya 4 - 17, ambao wamekatishwa masomo kinyume na sheria, hata hivyo amekuwa akiwaaminisha kuwa yeye ni Mungu anayeponya, kufufua watu na kutatua matatizo yao.
Jeshi la polisi lilipokea amri ya mahakama ya mwanzo mkuyuni tarehe 23.02.2022 iliyowataka polisi kumkamata mzazi wa kike wa mtoto Samir Ally Abbas aliyetakiwa kufikishwa mbele ya mahakama hiyo baada ya kesi ya msingi kusikilizwa.
Katika utekelezaji wa amri hiyo polisi walifika nyumbani kwa mtuhumiwa Dianna Edward Bundala ambapo ilidaiwa yupo mzazi wa kike wa mtoto huyo na mtoto aliyetakiwa kufikishwa mahakamani.
Hata hivyo baada ya askari kufika eneo la tukio mtuhumiwa aliongoza wafuasi wake kuwashambulia askari na kuwazuia kufanya kazi yao, ndipo askari waliondoka eneo hilo kwa nia ya kuepusha kutumia nguvu ambayo ingeweza kuleta madhara.
Tarehe 26.02.2022 Askari polisi walirudi nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kufanikisha ukamataji kwa mujibu wa sheria.
Aidha upelelezi wa kina unaendelea ili kubaini kiini cha watu hao kukusanyika katika nyumba ya mtuhumiwa ambayo sio nyumba ya ibadawala sehemu rasmi ya kongamano. Baada ya upelelezi kukamilishwa mtuhumiwa pamoja na washirika wake katika kutenda kosa watafikishwamahakamani ili hatua atahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Social Plugin