Mwanamke kutoka Mombasa mapema jana Alhamisi, Februari 3,2022 alipatikana amefariki dunia katika nyumba yake huko Bamburi baada ya kile kinachoaminika kuwa usiku wa mahaba na mwanaume asiyejulikana.
Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Alice Wasike inadaiwa alifariki dunia akimpakulia asali jamaa ambaye alihepa muda mfupi baada ya mama huyo kukata roho.
Kilichowashangaza zaidi maafisa wa polisi ni kuwepo kwa mwanamume mwingine aliyepoteza fahamu ambaye alikuwa juu ya maiti ya mwanamke huyo ilipopatikana.
"Mwanaume huyo bado amechanganyikiwa na hawezi hata kueleza jinsi alivyojipata juu ya mwanamke huyo. Tulijaribu kumuuliza lakini alionekana kuchanganyikiwa sana," jirani mmoja aliambia Citizen TV.
Mwanaume huyo baadaye alipelekwa katika kituo cha polisi.
Inaaminika kuwa Wasike, mama wa watoto watatu alimleta nyumbani mwanaume waliyekuwa na uhusiano wa mapenzi Jumatano, Februari 2,2022 lakini baadaye akatoroka mwanamke huyo alipokata roho wakirushana roho.
"Inashukiwa kuwa alikata roho wakifanya ngono kwa vile hakukuwa na majeraha yoyote mwilini mwake. Mwanamume ambaye inashukiwa walikuwa naye na asiyejulikana alikimbia kutoka eneo la tukio," sehemu ya ripoti ya polisi ilisema kama ilivyonukuliwa na K24.
Bado polisi wanafanya uchunguzi kubainisha ni vipi mwanaume huyo wa pili alivyojipata juu ya maiti ya mwanamke huyo.
Kamanda wa polisi wa Kaunti Ndogo ya Kisauni, Juma Fondo alisema kifo cha Wasike kilichukuliwa kama kifo cha ghafla kwa vile hakukuwa na alama zozote za kuashiria mtu alimdhuru.
Hata hivyo, uchunguzi wa tukio hilo tayari umeanza huku msako dhidi ya jamaa anayeshukiwa alikuwa na mama huyo akitafutwa.
Chanzo - Tuko News
Social Plugin