Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TBS YAWATAHADHARISHA WAFANYABIASHARA WANAOANIKA BIDHAA ZA VYAKULA KWENYE JUA

Afisa Uthibiti ubora, Bw.Baraka Mbajije akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ofisi za Makao Makuu ya TBS zilizopo Ubungo Jijini Dar es Salaam.


**************************


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewatahadharisha wafanyabiashara bidhaa za chakula zilizofungashwa yakiwemo mafuta ya kula kuweka ama kuanika kwenye jua kwani kunaweza kuleta madhara makubwa ya kiafya kwa binadamu.

Ameyasema hayo leo Afisa Uthibiti ubora wa bidhaa, Bw.Baraka Mbajije wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Makao Makuu ya TBS, Ubungo Jijini Dar es Salaam.

Amesema katika uchunguzi waliofanya wamebaini wengi wao wanaweka bidhaa nje kwenye jua ili wateja waweze kuona, sababu ambayo ni dhaifu kwani kunaweza kuhatarisha afya ya walaji.

Bw.Mbajije amesema kuwa kuweka bidhaa za vyakula nje kwenye jua inapelekea kuharibu kile chakula na ubora wa hiyo bidhaa unapungua hata kama bidhaa haijafika muda wake wa matumizi kuisha (Expire date).

"Bidhaa zote za chakula ndani yake zina kemikali mbalimbali ambazo ni za asili, lakini pia kwa bidhaa za viwandani kuna baadhi ya kemikali zinaongezwa zikiwa zinalengo nzuri, aidha kuongeza virutubisho au kuweka muda wa kutumika. Zile kemikali zilizopo kwenye chakula ukizihifadhi kinyume na utaratibu uliowekwa kwenye lebo na mtengenezaji au mzalishaji wa hicho chakula inaweza kupelekea hicho chakula kuharibika kwa haraka". Amesema

Aidha amesema wazalishaji wa mafuta ya kula huongeza virutubisho vya vitamini A kuhakikisha mtumiaji anatumia mafuta yaliyobora, hivyo mafua yakiwekwa kwenye jua Vitamini A huondoka kwa haraka hivyo mtumiaji nakuwa kwenye hatari ya kutumia mafuta yasiyo salama.

"Wafanyabiashara wanaoweka mafuta ya kula au bidhaa nyingine yeyote yenye virutubisho hivi kwenye jua wanatupelekea sisi Watanzania tunaokula vyakula tukose hiyo Vitamini muhimu ambavyo vilikuwa viimewekwa vizuri tu na wazalishaji". Amesema

Pamoja na hayo amesema chakula kilichopigwa na jua kinapoteza radha yake yya asili kwasababu ya shughuli za kemikali zilizkuwa zimefanyika katika kuandaa hicho chakula pia kuzalisha harufu ambazo hazikutarajiwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com