KATIBU wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Kenani Kihongosi
Na Dinna Maningo, Tarime
KATIBU wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Kenani Kihongosi,anatarajia kuwasili wilayani Tarime mkoa wa Mara ambapo atakagua miradi mbalimbali kikiwemo kituo cha Afya Sirari.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) Godfrey Fransis, amesema kuwa Katibu mkuu huyo anatarajia kuwasili kesho Februari,3,2022 na kupokelewa na viongozi wote wilaya ya Bunda,kisha atafika ofisi ya CCM wilaya ya Tarime kisha mtaa wa Iganana Sabasaba,Mwangaza na Nyamisangura kwa ajili ya zoezi la upandishaji wa Bendera.
Godfrey amesema kuwa baada ya zoezi la upandishaji wa bendera Katibu mkuu atafika kata ya Mwema na kata ya Bumera kukagua mradi wa Bwawa la Samaki,Mizinga ya nyuki na kituo cha afya Sirari.
Amesema kuwa baada ya kukagua miradi hiyo atatembelea shamba la kikundi na ghala la kuhifadhi mahindi, kisha kitafanyika kikao cha ndani cha chama ambapo katibu mkuu atahutubia wanachama wa chama hicho.
Hata hivyo vijana wa UVCCM wameeleza kufurahishwa na hujui wa katibu mkuu Taifa ambapo wamesema kuwa ujio wake utawezesha kuelezwa changamoto zinazowakabili vijana.
Hedson Mwita mkazi wa Nyamongo amesema kuwa ujio wake huwenda ukawezesha kuwasikiliza wananchi wa Nyamongo ambao walifanyiwa uthamini wa ardhi yao na mgodi wa Northa Mara, ili kupisha maeneo kwa ajili ya shughuli za mgodi lakini imepita zaidi ya miaka 10 hawajalipwa fidia.
Marwa Chacha mkazi wa kijiji cha Karakatonga kata ya Kwihancha amesema kuwa ujio wa katibu mkuu huwenda ukayafuta machozi yao kwani askari wa wanyamapori wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wamekuwa wakiwakamata na mifugo yao kutokana na mgogoro wa mipaka baina ya vijiji na hifadhi ya Serengeti ambapo wahanga wakubwa ni vijana.
Social Plugin