Na Emmanuel Mbatilo
KLABU ya Chelsea imeibuka Mabingwa wa Kombe la Dunia ngazi ya klabu mara baada ya kuichapa Palmeiras ya nchini Brazili kwa mabao 2-1 katika dakika 30 za nyongeza.
Chelsea ilianza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao Romelu Lukaku akipokea krosi kutoka kwa Hudson Odoi dakika ya 54 ya mchezo.
Dakika ya 64 ya mchezo Thiago Silva beki wa Chelsea aliunawa mpira ndani ya kumi nane akijaribu kuokoa mashambulizi kutoka kwa Palmeiras na kuamuliwa penati ambayo ilikwenda kupigwa na Raphael Veiga na kufanya matokeo kuwa 1-1 mpaka dakika 90.
Dakika 30 zilivyoongezwa Chelsea ilifanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji na dakika ya 116 mchezaji wa Palmeiras Luan Garcia nae akanawa mpira na kuamuliwa penati ambayo ilikwenda kupigwa na Kai Harvert na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi.
Social Plugin