Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, linawashikilia watu 10 kwa tuhuma za mauaji ya dereva taksi aliyekuwa anajulikana kwa jina la Respiciud Anastaz pamoja na Nicolaus Telesphory aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Mwanza (SAUT).
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani humo Ramadhan Ng’anzi, amesema katika tukio la kwanza watu wanne akiwemo mume na mke wanashikiliwa kwa tuhuma za kumuua Respicius Anastaz mwenye umri wa miaka 55 dereva taksi kwa kumkaba na kamba shingoni kisha kumchoma na visu shingoni na pia kumtoboa macho hadi kupelekea kufa.
Kamanda Ng’anzi amesema baada ya watuhumiwa hao kutekeleza mauaji hayo wakaenda kwa mganga wa kienyeji kufanyiwa dawa ili wasikamatwe ndipo askari walipowafuatilia na kufanikiwa kumkamata mganga na mkewe na kupeleka watuhumiwa kwenye tukio hilo kufikia wanne.
Katika tukio la pili Kamanda Ng’anzi amesema wanashikiliwa watu sita kwa tuhuma za kujichukulia sheria mkononi kwa kumpiga mawe na fimbo na kupelekea kifo kwa mwanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Augustine Mwanza, aliyekuwa anafahamika kwa jina la Nicholaus Telesphory mwenye umri wa miaka 25.
Chanzo - EATV
Social Plugin