Takriban watu 60 wameuawa siku ya Jumatatu katika mlipuko katika mgodi wa dhahabu katika kijiji karibu na Gaoua kusini-magharibi mwa Burkina Faso.
Makumi ya watu zaidi walijeruhiwa, wakiwemo wanawake na watoto
Ilitokea wakati vilipuzi vilivyohifadhiwa karibu na eneo la kuchimba dhahabu vilipolipuka, maafisa wa eneo hilo na mashahidi walisema.
Wengi wa watu waliojeruhiwa walihamishwa hadi hospitali ya mkoa ya Gaoua.
Mwendesha mashtaka wa mkoa aliyetembelea eneo la tukio alisema uchunguzi umeanzishwa kuhusu mkasa huo.
Ajali hutokea mara kwa mara katika shughuli za uchimbaji madini ambazo hazijaidhinishwa katika baadhi ya nchi za Afrika, huku udhibiti wa usalama mara nyingi ukiwa mdogo au haupo kabisa.
Chanzo - BBC Swahili
Social Plugin