Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

FAINALI YA UEFA YAHAMISHWA KUTOKA URUSI...SASA KUCHEZWA PARIS



Fainali ya Ligi ya Mabingwa 2022 itachezwa jijini Paris baada ya Urusi kuvuliwa uenyeji wa mechi hiyo kufuatia uvamizi wa taifa hilo nchini Ukraine. Fainali ya shindano hilo la kifahari la vilabu barani Ulaya ilitarajiwa kuchezwa huko St Petersburg mnamo Mei 28.

Kufuatia mkutano wa Ijumaa, Uefa ilithibitisha kuwa mechi hiyo haitachezwa katika uwanja wa Gazprom Arena. Badala yake shirikisho la soka barani Ulaya limeamua kuwa litafanyika katika uwanja wa Stade de France jijini Paris.

Uefa “imemshukuru sana” Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa “msaada wake binafsi na kujitolea kuwa mwenyeji wa mchezo huo wa kifahari zaidi wa klabu ya Ulaya kufuatia mgogoro huo usio na kifani”.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com