WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima,akizungumza katika kikao cha kamati ya Mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) ya Mkoa wa Dodoma Kilichofanyika leo Februari 15,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima,akielezea jambo kwa washiriki wa kikao cha kamati ya Mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) ya Mkoa wa Dodoma Kilichofanyika leo Februari 15,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima,akionyesha Mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) ya Mkoa wa Dodoma Kilichofanyika leo Februari 15,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula,akielezea mikakati ya wizara hiyo katika kikao cha kamati ya Mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) ya Mkoa wa Dodoma Kilichofanyika leo Februari 15,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima,akimsikiliza Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw.Benard Abraham,akizungumzia mkakati wa Mkoa katika kutekeleza Mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) Mkoa wa Dodoma wakati wa kikao hicho Kilichofanyika leo Februari 15,2022 jijini Dodoma..
Mratibu wa MTAKUWWA ngazi ya Taifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Happiness Mugyabuso,akitoa salam za ofisi hiyo wakati wa kikao cha kamati ya Mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) Mkoa wa Dodoma Kilichofanyika leo Februari 15,2022 jijini Dodoma.
Baadhi wa Watendaji wa Wizara hiyo wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima (hayupo pichani) katika kikao cha kamati ya Mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) Mkoa wa Dodoma Kilichofanyika leo Februari 15,2022 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima (hayupo pichani) katika kikao cha kamati ya Mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) Mkoa wa Dodoma Kilichofanyika leo Februari 15,2022 jijini Dodoma.
....................................................
Na.Alex Sonna,DODOMA
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dk.Doroth Gwajima amezielekeza kamati za ulinzi wa wanawake na watoto ngazi ya Mkoa kuandaa mikakati madhubuti iliyoboreshwa itakayosaidia kuimarisha utendaji kazi kwa lengo la kutokomeza vitendo vya ukatili nchini.
Dk.Gwajima ametoa maagizo hayo wakati wa kikao kazi na viongozi wa Mpango wa Kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na Watoto (MTAKUWWA) Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo Februari 15,2022 jijini Dodoma
Waziri Gwajima amesema kamati za ulinzi wa wanawake na watoto ngazi ya Mkoa zinatakiwa kuandaa mikakati madhubuti iliyoboreshwa na itakayosaidia kuimarisha utendaji kazi ikiwemo kukamilisha uundwaji wa Kamati hizo na kuzijengea uwezo ili zitekeleze majukumu yao ipasavyo kwa lengo la kutokomeza vitendo vya ukatili.
Pia,amezielekeza kuhakikisha rasilimali fedha zinatengwa na kutolewa kwa ajili ya utekelezaji wa afua za MTAKUWWA kama inavyoelekezwa katika Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali unaotolewa kila mwaka na Wizara ya Fedha na Mipango.
“Kubainisha wadau wanaotekeleza afua mbalimbali katika Mkoa zinazolenga kupambana na vitendo vya ukatili na uimarishaji wa uchumi wa kaya ili kushirikiana nao katika jitihada za kutokomeza vitendo vya ukatili kwenye jamii ikiwemo kudhibiti wimbi la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani,”amesema.
Katika hatua nyingine,Waziri Gwajima amezitaja changamoto zinazoathiri jitihada za utekelezaji wa mpango huo kuwa ni pamoja na utendaji usioridhisha wa kamati za ulinzi wa Wanawake na Watoto hususan kwenye ngazi za Mamlaka za Serikali za Mitaa/vijiji.
“Utengaji na utolewaji duni wa fedha za utekelezaji wa afua za MTAKUWWA katika ngazi zote,ushirikiano mdogo wa kiushahidi kutoka kwa waathirika wa vitendo vya ukatili dhidi ya watuhumiwa hususan watu au ndugu wa karibu na hivyo kusababisha kesi nyingi kushindwa kutolewa maamuzi na watuhumiwa kuachiwa huru,”amesema
Ameitaja changamoto nyingine ni upungufu wa watendaji wa kada mbalimbali zinazohusika moja kwa moja katika kushughulikia masuala ya ukatili nchini kama vile Maafisa Ustawi wa Jamii, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Polisi na Wanasheria hususan katika ngazi za kata na vijiji au mitaa.
“Uwepo wa mila na desturi zenye madhara ndani ya jamii zetu zikiwemo za ukeketaji na ndoa za utotoni ambazo zimeendelea kumkosesha haki za mtoto wa kike na kuathiri maendeleo na ustawi wake,”amesema.
Amesema mpango huo una lengo la kupunguza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2021-22 ambapo, ili kufikia lengo hilo, Serikali kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo imekuwa ikitekeleza afua mbalimbali zinazolenga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupitia maeneo nane.
Waziri Gwajima amesema kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto 18,186 zimeanzishwa ngazi ya Taifa, Mkoa, Halmashauri,ambapo kata na Kijiji/Mtaa mwaka 2020/21 ikilinganishwa na 16,343 mwaka 2019/20, sawa na ongezeko la Kamati 1,843.
Amesema madawati ya jinsia na watoto yameanzishwa katika Vituo vya Polisi ambapo hadi Desemba 2021 yalikuwa 423 na Madawati Matano (5) ya Jinsia (5) katika Taasisi za Elimu ya Juu na Kati.
Amesema huduma za msingi na hifadhi ya dharura kwa waathirika wa ukatili zimeendelea kutolewa katika nyumba salama 9 katika mikoa ya Arusha (2), Iringa (1), Kigoma (1), Mara (2), Manyara (1), Morogoro (1) na Mwanza (1).
Amesema jumla ya watoto 167 (wavulana 111 na wasichana 56) na wanawake 269 walipata huduma.
“Serikali imeendelea kuwawezesha kiuchumi wanawake, vijana pamoja na watu wenye ulemavu kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri,”amesema
Amesema katika kipindi cha Julai 2020 hadi Aprili 2021, jumla ya mikopo (isiyo na riba) ya Tsh bilioni 27.07 ilitolewa kwa wanawake ikilinganishwa na Tsh bilioni 23.86 zilizotolewa mwaka 2019/20.
Kwa upande wake,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dk. Zainabu Chaula,amewahimiza watendaji wa Mpango huo kuhakikisha wanatimiza wajibu wao na kuondoa vitendo vya ukatili kwenye maeneo yao.
Mratibu wa MTAKUWWA ngazi ya Taifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Happiness Mugyabuso,amesema kuwa watashirikiana na wadau mbalimbali katika mapambano ya ukatili na kuendelea kuimarisha mifumo ya serikali.
Naye,Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Afisa Kilimo Mkoa wa huoa,Benard Abraham amesema suala la ukatili dhidi ya watoto na wanawake ni suala mtambuka ambapo sababu kubwa inayosababisha ni kiwango cha uchumi kuanzia ngazi ya kaya.
Social Plugin