Waziri wa Nishati na Madini wa Burundi, Ibrahim Uwezeye (kulia) na Waziri wa Madini nchini, Dotto Biteko wakikata utepe wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2022, Dar es Salaam leo.
Waziri wa Nishati na Madini wa Sudan Kusini, Martin Gama Abucha, (wa pili kushoto) akipata maelezo ya shughuli za kampuni ya madini ya Barrick kutoka kwa Meneja Uhusiano, Neema Ndossi (katikati) wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya kimataifa ya uwekezaji katika sekta ya madini Tanzania 2022 yanaoendelea jijini Dar es Salaam (kulia) ni Ofisa wa Barrick Abela Mutiganzi
Mmoja wa wageni akisaini kitabu baada ya kutembelea banda la kampuni ya madini ya Barrick.
***
Kampuni ya madini ya Barrick inashiriki katika mkutano wa kimataifa ya uwekezaji katika sekta ya madini Tanzania 2022 unaofanyika jijini Dar es Salaam katika viwanja vya ukumbi wa Mwalimu Nyerere ukiambatana na maonesho ya wadau mbalimbali wa sekta ya madini.
Maonesho haya yalizinduliwa na Waziri wa Nishati na Madini wa Burundi, Ibrahim Uwizeye, akishirikiana na mwenyeji wake, Waziri wa Tanzania, Dk. Doto Biteko.
Barrick ni moja ya wadhamini wa mkutano huo
Social Plugin