Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Prof.Lawrence Museru akiwa pamoja na wataalamu wa afya akionesha cheti cha Ithibati ya ubora (ISO 15189:2012) kutoka Shirika la Viwango vya Ukaguzi kimataifa kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADCAS) ambacho wamepatiwa hospitali hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Prof.Lawrence Museru akionesha cheti cha Ithibati ya ubora (ISO 15189:2012) kutoka Shirika la Viwango vya Ukaguzi kimataifa kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADCAS) ambacho wamepatiwa hospitali hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Prof.Lawrence Museru akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila leo tarehe 10/02/2022 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
***********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Maabara ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila imepata cheti cha Ithibati ya ubora (ISO 15189:2012) kutoka Shirika la Viwango vya Ukaguzi kimataifa kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADCAS) na kuingia katika orodha ya maabara zinazotoa huduma bora Duniani.
Ametoa taarifa hiyo leo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Prof.Lawrence Museru wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini dar es Salaam.
Prof.Museru amesema ithibati hiyo imetokana na SADCAS kujiridhisha na ubora wa vipimo na majibu yanayotolewa na maabara ya Hospitali ya Mloganzila ambapo uliangalia na kuthibitisha vitu mbalimbali ikiwemo miongozo, uwezo wa wataalamu, ufanisi wa vifaa tiba na miundombinu ya maabara kwa aina kumi na saba (17).
"Kuaminika kkwa ubora wa vipimo na majibu kimataifa, sampuli ya vimelea vitakavyopimwa katika maabara hii yanaweza kutumiwa na mamlaka au Taasisi yoyote Duniani". Amesema Prof.Museru.
Amesema Maabara hiyo itakuwa ni kituo cha mafunzo na utafiti wa vimelea mbalimbali kutokana na ubora wa huduma zake.
Aidha amesema Wizara ya Afya iliweka mikakati mbalimbali ya kuboresha huduma za maabara nchini kufikia kiwango cha kimataifa yaani ithibati ya Ubora Kimataifa ambapo maboresha hayo yalilenga kuboresha maabara 25 zinazotoa huduma za kimatibabu ya afya hapa nchini.
"Maabara ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila ni miongoni mwa maabara 25 zilizokuwa zikitekeleza sera hiyo ambapo imefanikiwa kufanya vizuri na kushika nafasi ya kwanza kati ya maabara zote 25 kwa kuwa na wigo mpana wa vipimo 17 vilivyopata ithibati ukilinganisha na maabara nyingine". Amesema
Social Plugin