Mfano wa chupa zenye sumu
**
Kijana aliyejulikana kwa jina la Ginasa Petro (30) mkazi wa kijiji cha Kayenze, kata ya Kafita wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita amejiua kwa kunywa sumu ya Panya baada ya mke wake Sarah Jeremia kukataa kurudi kuishi naye baada ya hapo awali kuondoka kutokana na mgogoro wa kimapenzi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba wivu mkubwa ndiyo uliopelekea mwanaume kuchukua maamuzi hayo
Ameshauri wanandoa kuwa wanapaswa kuwaona viongozi wao wa dini ili kusuluhisha changamoto zao na si kujitoa uhai.
Social Plugin