DC KISWAGA ARIDHISHWA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ELIMU, AFYA NA MAJI KAHAMA


Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akiangalia mabomba ya mradi wa maji Mwime

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga ameeleza kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta za elimu, afya na maji inayotekelezwa na fedha zinazotolewa na serikali zikiwemo pesa za UVIKO 19 wilayani Kahama.

Hayo yamejiri leo Alhamisi Februari 17,2022 wakati Kiswaga akitembelea na kujionea miradi inayotekelezwa kwa fedha za serikali zinazotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan tangu alipoingia madarakani.

Akiongea na Wandishi wa habari katika miradi hiyo aliyotembelea katika Manispaa ya Kahama na Halmashauri ya Msalala amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji kwa kiwango bora pamoja na matumizi ya fedha hiyo huku akibainisha kuwa mpaka sasa kuna shilingi bilioni 5 za miradi itakayokamilika ifikapo mwezi Aprili 2022.

Akianzia katika mradi wa ujenzi wa jengo Idara ya Matibabu ya Nje (OPD) la ghorofa moja katika hospitali ya Manispaa ya Kahama  linalojengwa kwa mapato ya ndani kwa kiasi cha shilingi Bilioni 3.5  lilipofikia sasa ambapo serikali pia imetoa zaidi ya shilingi. 1 bilioni amesema amefurahishwa na mradi huo.

Aidha amesema kwa upande wa sekta ya elimu katika ujenzi wa Shule ya sekondari ya Mama Samia , kata ya Majengo mjini Kahama iliyokamilika pamoja na Shule ya sekondari ya kata ya Kagongwa inayoendelea kujengwa zilizopata zaidi ya shilingi bilioni moja katika kuunga mkono nguvu za wananchi umekwenda vizuri.

Kwa upande wa miradi ya huduma ya kusambaza mtandao wa maji inayotekeleza na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA) kwa thamani ya shilingi Bilioni 7 zilizotolewa na Serikali , Kiswaga asema utekelezaji huo unakwenda kwa kasi hali ambayo imewalizisha wananchi wa eneo la Mwime na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hiyo.

Miradi aliyotembelea ni ujenzi wa Idara ya Matibabu ya Nje (OPD) hospitali ya Manispaa ya Kahama ambapo serikali imetoa kiasi cha zaidi ya bilioni moja , shule ya sekondari Mama Samia iliyopata shilingi Milioni 180 kutokana na kuwa wananchi walikuwa wamejenga maboma 10 ya vyumba vya madarasa,Kagongwa sekondari iliyopata shilingi milioni 500 , mradi wa maji Mwime kiasi cha milioni 518 , na kuona mgodi wa dhahabu wa kati wa Kampuni ya CANUCK Mwakata toka uanze 2021 ambapo umeweza kuchangia mapato ya serikali kiasi  cha shilingi milioni 240 kwa mujibu wa Afisa madini mkazi wa mkoa wa kimadini wa Kahama Jeremiah Hango.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na waandishi wa habari wakati akitembelea miradi mbambali leo
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Mhe. Anderson Msumba
Muonekano wa jengo la Idara ya Matibabu ya Nje (OPD) la ghorofa moja katika hospitali ya Manispaa ya Kahama 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akiangalia mabomba ya mradi wa maji Mwime
Muonekano wa moja ya majengo ya shule ya Sekondari Mama Samia
Maboma ya majengo ya shule ya sekondari Kagongwa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post